Mafanikio ya biashara hayaji kwa usiku mmoja (overnight), lakini ukiwa na nia ya kufanikiwa, siku moja ndoto zako zitatimia.Mhandisi
Patrick Ngowi, anaweza kuwa kati ya wafanyabiashara wachache nchini
ambao ndoto zao za kuwa wafanyabiashara wakubwa, zimetimia angali wakiwa
bado vijana wadogo.Ngowi ambaye wazazi wake ni walimu wa shule za
sekondari, alianza safari yake ya biashara baada ya kumaliza kidato cha
sita katika Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es Salaam wakati huo
akiwa na miaka 19.Anasema kuwa baada ya kumaliza kidato cha sita
alihitajika kukaa nyumbani mwaka mmoja wakati akisubiri matokeo ili
kwenda chuo kikuu.“Sikupenda kukaa nyumbani bila kufanya kitu chochote, nilitamani kufanya kitu chochote kitakachoniweka bize,” anasema.
Mama alinikopesha mtaji wa Sh2.3.
Anasema
mama yake, Emmy, alimkopesha Sh2.3 milioni, lakini sasa Kampuni yake ya
Helvetic Solar Contractors sasa inaingiza mapato ya Sh4 bilioni kwa
mwaka.
Baada ya kupata fedha hizo, anasema rafiki yake mwingine
ambaye kwake ni sawa na kaka, alimpa tiketi ya ndege pamoja nyaraka zote
na kusafiri mpaka China ambako alinunua simu kuja kuziuza Tanzania.
“Biashara ile ilikuwa na faida, sisi tulikuwa tunanunua simu moja kwa dola mbili za Marekani tunakuja kuuza Dola 18.“Mwanzo
kabisa nilikuwa na wazo tu na tiketi ya kwenda China, baada ya
kutembelea China, niliamua kutafuta fedha kwa ajili ya kufanya biashara
ya kuuza simu za mkononi, kutokana na faida niliyopata baadaye nilikuwa
na uwezo kufungua kampuni.“Msingi wa yote haya ni mama yangu pamoja na na muungwana mwingine waliokubali kunipa mkopo ambao haukuwa na riba,” anasema.Ni
wazi kuwa, baada ya Ngowi kuona biashara ya simu haitamsaidia kufikia
ndoto zake, aliamua kusoma masomo ya umeme wa jua katika Chuo Kikuu cha
Dezhou mchini China.
Lakini pamoja na hayo Kampuni ya Ngowi,
Helvetic Solar Contractors, mwaka huu imeshika namba moja kati ya
kampuni bora 100 za kati zinazokua kwa kasi (Top 100 Mid-sized Companies
2012). Wakati Ngowi akisoma alikuwa akiendelea na biashara ya kuuza
simu.Mgao wa umeme wampatia mabilioniKwa mujibu wa taarifa za
Serikali, kati ya zaidi ya Watanzania milioni 40, asilimia 14 pekee ndio
wanaotumia umeme wa gridi ya taifa.
Kutokana kuliona hilo, kabla ya kuhitimu masomo yake, aliamua kusajili kampuni yake ya Helvetic Solar Contractors.Mwaka
2008 akiwa na miaka 23, alirejea nchini akiwa mhitimu katika fani ya
masuala ya umeme wa jua huku akiwa tayari amesajili kampuni yake.
Pamoja
na kuwa na akiba aliyoweka kutokana na mauzo ya simu, bado alihitaji
mtaji zaidi ili aweze kufanya biashara hiyo ya kuagiza na kufunga sola.Wakati
akifikiri hilo, alipata rafiki mwingine ambaye ni Raia wa Uswiss,
Philippe Glauser ambaye alikubali kumkopesha kiasi cha fedha bila riba.
“Hivyo
ndivyo kampuni ilivyoanza, wakati huo ikiwa haina hata gari na mimi
nikiwa mwenyewe, kwa mwaka wa kwanza niliweza kutengeza faifa ya Sh30
milioni,” anasema.
Hivi sasa anasema kampuni yake ina magari 14, Land cruiser saba, pickup tatu, Magari mawili ya madogo (salon) na VX mbili.Pia anasema kampuni hiyo kwa sasa ina wafanyakazi 16, nane kati yao wakiwa wamesomea mambo ya umeme.Pamoja
na kuwa na wazo pamoja na kufungua kampuni, anasema watu wengi kutokuwa
na uelewa wa kutosha juu ya faida na matumizi ya nishati hiyo ilikuwa
ni changamoto kwake alipokua akianza kazi.“Daima mwanzo ni ngumu.
Mwaka 2007 siyo watu wengi walikuwa wanajua umuhimu wa nishati ya jua
au jinsi inavyoweza kutumika, mgao wa umeme wa mwaka 2011 ulifanya watu
waanze kutafuta vyanzo vingine mbadala vya nishati na kwa wakati huu
sisi pekee ndio tuliokuwa miongoni mwaka kampuni kubwa zilizoweza kutoa
majibu ya tatizo hilo,” anasema.
Anasema baada ya kutimia mwanya huo
wa mgao wa umeme, wamepata soko zaidi baada ya kutoa bidhaa bora, kwa
wakati na vifaa vyao kuwa na dhamana ya muda mrefu kwa wateja. “Kwa
sasa sisi ni kati ya kampuni maarufu za kutoa huduma hii Tanzania, pia
tumechaguliwa kusambaza bidhaa hii katika nchi nyingine za Afrika
Mashariki, tuna timu kusambaza na kufunga vifaa hivi,” anasema.
Anasema ili kuboresha huduma zao wanashirikiana na kampuni kutoka nchi za magharibi lengo likiwa ni kufanya vizuri sokoni.Ngowi
anasema kampuni yake ilianza kwa kutumia vifaa kutoka China, lakini kwa
sasa wana tumia vifaa Marekani, Ujerumani, hispania na Israeli.Ngowi kuwasomesha wafanyakazi wake Ujerumani.Anasema kwa kuwa mafanikio ya kampuni yanatokana na wafanyakazi wake, moja kati ya mambo wanayozingatia ni kuwaendeleza kielimu.Ngowi anasema, wanafikiria kuwapeleka Ujerumani kwenye mafunzo ili wafikie viwango vya kimataifa.
Anasema
mbali na ofisi ya Arusha waliloanza nayo mwaka 2007, sasa wamefungua
ofisi Moshi, Dar es Salaam na mwaka 2013 watafungua nyingine Mwanza.“Wito
wangu kwa vijana, siku zote wajue kuwa jambo la msingi ni kuwa na wazo
la kile unachotaka kufanya, kuwa na mtaji bila wazo ni sawa na bure,
kuwa na wazo kisha panga namna ya kulitekeleza, baada ya hapo muombe
Mungu atakuongoza,” anasema Ngowi.Pia anasema elimu ya ujasiriamali
kwenye shule za msingi na sekondari ni moja ya vitu muhimu vinavyoweza
kuwainua wajasiriamali nchini.
Post a Comment