Steven Wambura |
Steven Wambura ni mmoja wa vijana hao ambapo sasa ni msanii wa muziki wa Injili, huku muziki wake ukiwa ni wa bolingo na rumba.Kipaji
cha Wambura kilianza kuonekana mwaka 1987 alipokuwa akiimba kwaya
katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Bethel Kijenge mkoani
Arusha.
“Wakati huo nilikuwa bado nikisoma, na masomo yangu
yalikuwa magumu, nakumbuka nilipigwa na wazazi na wakati mwingine
kulazwa njaa kutokana na kujihusisha na masuala ya muziki,” anasema.
Wambura anasema kuwa kipindi hicho wazazi wake
walikuwa hawapendi ajishughulishe na muziki na kwamba mara zote walikuwa
wakimsisitizia asome.
“Siwezi kuwalaumu, inawezekana walikuwa wanaogopa
kwa sababu kulikuwa na dhana kuwa muziki wa Tanzania haulipi, lakini
sasa muziki ndiyo unaendesha maisha yangu,”anasema.
Anaeleza kwamba baada ya kumaliza kidato cha nne
mwaka 1993, aliendelea kuimba kwaya hadi mwaka 1994, alipoamua kuanzisha
bendi yake iliyoitwa Chipukizi, ambayo alidumu nayo hadi mwaka 1997.
“Bendi haikudumu sana na mwaka 1998 niliajiriwa
kwenye duka moja la dawa mkoani Arusha. Mwaka uliofuata niliamua kwenda
nje kutafuta maisha,” anasimulia.
Anasema kuwa mwaka 2003 alirudi nchini na
kuendelea na shughuli za uimbaji, ambapo aliamua kutoka kwenye mfumo wa
kwaya na kuwa muimbaji binafsi.
Studio ikizinduliwa kwa maombi na baadhi ya viongozi wa makanisa Dar. |
Wambura anaeleza kuwa wakati akiendelea na
shughuli za uimbaji binafsi, aliamua kuokoka mwaka 2005 na Mungu
kumjalia kutoa albamu mbili ambazo ni Bwana ndiye bwana na Roho wa
bwana.
Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hizo ni
Bwana ndiye bwana, Bwana ndiye mchungaji wangu, Ita jina la yesu,
Upendo, Nilitembea tembea, Bwana u sehemu yangu, Usilie tena na Nataka
nikujue.
“Albamu zote hizi zilifanya vizuri sokoni na kunivutia niendelee na muziki,”anasema.
Hata hivyo, anasema kuwa licha ya mafanikio aliyoyapata katika uimbaji, alikuwa na ndoto ya kumiliki studio yake binafsi, ambayo itajikita katika uandaaji wa muziki, vipindi maalumu pamoja na mahubiri.
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Kinondoni Revival Church (KRC) TAG Askofu Dr Rogathe Zakayo Swai akipiga baadhi ya vyombo katika studio ya Steven Wambura . |
Hata hivyo, anasema kuwa licha ya mafanikio aliyoyapata katika uimbaji, alikuwa na ndoto ya kumiliki studio yake binafsi, ambayo itajikita katika uandaaji wa muziki, vipindi maalumu pamoja na mahubiri.
“Msukumo wa kuanzisha studio hii na kuwekeza kiasi
kikubwa cha fedha lengo lake siyo kufanya biashara, bali kuujenga
ufalme wa Mungu na kuwasaidia wengine kutimiza ndoto zao,”anasema
Wambura.
Post a Comment