MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), amemfutia kesi mmoja wa washtakiwa
waliojumuishwa katika kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake.Pia katika
kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, hakimu
ameuamuru upande wa mashtaka uache utaratibu wa kumwingiza mahakamani
mshtakiwa wa kwanza, Sheikh Ponda akiwa amefungwa pingu.
Aliyefutiwa mashtaka jana ni mshitakiwa wa 35 katika kesi hiyo, Rashid Omar.Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka ndiye aliyetoa taarifa kuhusu uamuzi huo wa DPP wakati wa usikilizwaji wa maelezo ya awali wa kesi hiyo jana.

Sheikh Ponda Issa Ponda akizungumza na wakili wake
Watuhumiwa wakiwa mahakamani
Askari maalumu wakiwa tayari kwa varangati lolote
Hapa fanya fujo uone - Jamaa wana kiu kwelikweli na chafuko lolote .
Doria kama kawa
Ulinzi kama dawa vile , hapiti mtu pasiko kukaguliwa
Du hadi inatishaa , cheki hapa...
Ulinzi kama kawaida ulikuwa mkali , ili kudhitibi usalama wakati wa kesi ikisomwa.
Picha na Taarifa kwa hisani ya gazeti la mwananchi na blog ya http://richard-mwaikenda.blogspot.com/
Post a Comment