Social Icons

Loading...

MMOJA AUAWA KATIKA VURUGU ZA WAMACHINGA NA MGAMBO MWANZA

MWENDESHA mkokoteni amekufa na na watu wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi katika vurugu kubwa zilizozuka  kati ya askari mgambo wa Jiji  la Mwanza na wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) Jijini Mwanza leo.
 
Mapambano hayo yalianza majira ya saa 4:00 ausubuhi na kusababisha maduka kufungwa pamoja na biashara mbalimbali kutofanyika.
Tukio la kuuawa kwa mwendesha mkokoteni  huyokatika soko kuu la Jiji la Mwanza, lilitokea baada ya askari mgambo kuwafyatulia risasi machinga waliokuwa wakipambanan kuzuia mgambo hao wasichukue mali zao .
 Mgambo hao walifika eneo hilo la stendi kuu ya zamani mabasi ya Tanganyika basi kisha kuzoa mali za wafanyaibishara hao kwa madai kuwa wanafanya shughuli hizo kinyume cah sheria katika ameneo yasiyoruhusiwa an halmashauri ya jiji la Mwanza. 
 
Kutokana hali machinga hao walipinga bidhaa zao walizopanga chini (mali) kuchukuliwa na mgambo hao wa jiji ndipo mmoja wao aliyekuiwa na bunduki aina ya short gun akawafyatulia risasi ambazo zilimpiga kuli huyo upande wa kushoto na kufariki dunia papo hapo.
 Mbali nakuli huyo derebva wa gari moja aina ya canter naye alijeruhiwa sikio la upande wa kushoto na machinga mmoja kujeruhiwa mkono wa kushoto kwenye kiwiko.

 Kaimu kamnda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ofisa Mnadhimu (SO) SSP Lilian Matola , alitihibitisha kutokea kwa vurugu hizo ambazo zilisababisha kifo bna majeruhi na kwamba jeshi hilo lilingia mtaani kutuliza ghasia hizo ambazo zilidumu kwa saa nne.

 Alisema askari mgambo wa jiji wanaotuhumiwa kusababisha kifo na majeruhi hao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.

 Kwa mujibu wa SSP Matola , mgambo hao wa jiji walitumia risasi hizo za moto kwa nia ya kujihami na kundi la wafanyabiashara hao ambao walikuwa wakiwashambulia kwa mawe.

 Alisema majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC ) ya jijini hapa, huku mwili wa marehemu huyo ukihifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali hiyo.

 Aidha Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula, aakizungumza na wandishi wa habati kwenye ukumbi wa jiji jana jioni alisema hakukuwa na opereshani maalumu ya kuwaondo machinga katika meneo hao bali shughuli za kawaida za halmashauri hiyo kuhakikisha jiji liakuiwa safi.

 Alisema kuwa kilichotokea ni kutokana na mgongano wa mawazo kati ya mgambo na machinga hali iliyosababisha askari hao wa jiji kutumia risasi za moto,hivyo akaomba radhi kwa tukio hilo na kutoia pole kwa ndugu na familia za marehemu pamoja na ndugu wa majeruhi na majeruhi wenyewe.

 Meya huyo alisema vurugu hizo hazihusiani na chama chochote cha siasa bali ni tukio la bahati mbaya, hivyo uongozi wa jijini unasikitishwa mno na tukio hilo.

“Niseme kuwa vurugu hizi hazihusiani na chama chochote, si chama change cha CCM ama watani wetu CHADEMA, ni tukio la bahati mbaya.Kila tunapofanya operesheni tunahusiha vyombo vya usalama, wamchinga wenyewe na madiwani,”alisema Mabula na kuiongfeza kuwa ;

“Inasemekana kwamba risasi za moto zilitumika katika zoezi hilo na kusababisha watu kupoteza maisha na baadhi kujeruhiwa.Kwa sasa suala hili liko katika vyopmbo vya ulinzi na usalama kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kitu gani kimetokea.”

Alikiri kuwa askari walioajiriwa na jiji wamepitia mafunzo ya mgambo,hivyo kitendo cha kutumia silaha ama matumizi mabaya ya silaha ni kinyume cha sheria.Ikitihibtika kuwa walifanya makosa hayo sheria itachukua mkondo wake.

 Alisema watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa na jeshi la polisiu kwa ajili ya kuchunguza kama walitumia silaha vibaya.

 Hata hivyo Mabula alisema kuwa pamoja na jiji kuwa sheria ndogo ndogo bado haliwezi kuwaondoa machinga katika maeneo ya katikati ya jiji kwa kuwa linawatambua kutokana na kazi yao ya ujasiriamali inayowapa kipato.

leo kutwa nzima ukiondoa soko kuu biashara mbalimbali zikiwemo za maduka na aina zingine zilishindikana kufanyika kutokana na vurugu hizo pamoja na jeshi la polisi kutumika kuwatawanya kwa amani machinga hao.

 Vurugu kama hizo zimewahi kutokea mara kadhaa na kusababisha uharibifu wa mali,kuchoma moto magari , kuvunja milango na viio vya baadhi ya maduka na kupora mali,ambapo watru kadhaa walijeruhiwa na wengine kufariki kwa kupigwa risasi za moto.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top