KITUO cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini kinatarajia
kuonyesha mechi nane za watani wa jadi kutoka sehemu mbalimbali duniani
mwezi Oktoba ikiwamo mechi ya Simba na Yanga.
Kati
ya mechi hizo za watani wa jadi itakayoanza kuonyeshwa itakuwa ni mechi
kati ya Simba na Yanga hapo Oktoba 3 kupitia chaneli ya SuperSport
9east.
Crew ya SuperSports iliyoko Tanzania wiki hii. |
Meneja uhusiano wa MultiChoice Tanzania,
Barbara Kambogi alisema hayo wakati alipotembelea ofisi za Mwananchi
Tabata Relini jijini Dar es Salaam, mechi nyingine za watani wa jadi
zitakazoonyeshwa na kituo cha SuperSport mwezi Oktoba ni kati ya
Barcelona dhidi ya Real Madrid (Hispania), Boca Juniors dhidi ya River
Plate (Argentina) na Borussia Dortmund dhidi ya Schalke (Ujerumani).
Mechi
nyingine ni kati ya Ajax Amsterdam dhidi ya Feyenoord Rotterdam
(Uholanzi), Liverpool dhidi ya Everton (England), Inter Milan dhidi ya
AC Milan (Italia) na CSKA dhidi ya Spartak (Russia).
Pia
Kambogi alisema kuanzia leo kituo cha SuperSport kitaanza kuonyesha
baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya Tanzania, ambapo leo itaonyeshwa mechi
kati ya Azam dhidi ya JKT Ruvu kuanzia saa 11:45 jioni.
Mechi
nyingine zitakazoonyeshwa na SuperSport ni kati ya Simba dhidi ya
Tanzania Prisons kesho, Yanga dhidi ya African Lyon siku ya Jumapili,
JKT Ruvu dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya Jumatatu kabla siku ya Jumatano
kuonyesha mechi ya Simba na Yanga.
Naye
mchambuzi wa soka katika kituo cha SuperSport, Thomas Mhlambo raia wa
Afrika Kusini aliyekuwa ameambatana na Kambogi alisema muda siyo mrefu
Tanzania itakuwa na wachezaji wa soka wengi wanaocheza soka katika nchi
mbalimbali ulimwenguni.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
(kulia) akizungumza na watangazaji maarufu wa Kampuni ya Super Sport ya
Afrika Kusini, Thomas Mlambo (kushoto) na Thomas Kwenaite wakati wa
hafla ya uzinduzi wa kampuni hiyo kuanza kwa majaribio kutangaza baadhi
ya michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom nchini katika hafla iliyofanyika Dar
es Salaam jana
Post a Comment