JULIUS Kaisari alipata kutamka; “ My wife ought not even to be under suspicion”- Kwamba mke wangu hapaswi hata kutuhumiwa.
Kaisari alikuwa akijibu swali la kwa nini alimwacha mkewe Pompeia kwa tuhuma za kwenda kinyume na mienendo mema ya ndoa.
Ndio, tuhuma peke yake, hata kabla ya kuthibitishwa, zilitosha kwa Kaisari kumwacha
mkewe ili alinde hadhi na heshima yake. Akiamini, kuwa wenye kuhusiana
na walio katika uongozi na utumishi wa umma hawapaswi kutuhumiwa kwa
kutenda yalo maovu.
Hapa kwetu haijapata kutokea, kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa kwenye tuhuma nzito ya rushwa kama ilivyo sasa. Ni vema tukatambua sasa uzito wa jambo hili; kwamba kwa Waziri mwenye dhamana kutoa hadharani tuhuma za wabunge kuhongwa ni kashfa kubwa.
Si
tu kwa wabunge husika, bali kwa Bunge zima, kwa Serikali nzima, kwa
nchi nzima. Hakuna dawa nyingine ya kuondokana na kashfa mbaya kama hiyo
isipokuwa kwa wenye kutuhumiwa kukaa pembeni kwa maana ya kujiuzulu ili
kupisha uchunguzi wa kina na ripoti yake kwa Bunge na umma.
Maana,
hapa kuna mawili yanayotarajiwa kutokea pindi ripoti ya uchunguzi
itakapotoka; ama kuwatia hatiani watuhumiwa au kuwasafisha na tuhuma
hizo. Hilo la kwanza likitokea ni vema na busara likaendana na hatua
kali za kinidhamu na kisheria kwa wahusika hata kama tayari
wameshajiuzulu.
Lakini,
likitokea la pili, kwamba Tume iliyoundwa kuchunguza kadhia hiyo
ikawaona watuhumiwa hawana hatia, hivyo kuwasafisha, basi, Waziri mwenye
dhamana aliyetoa tuhuma hizo hadharani na watendaji wenzake wakuu wenye
kuhusika na taarifa ya Waziri wanapaswa wajiuzulu mara moja. Ni kwa
vile, watakuwa wamesema uongo.
Chanzo: Raia Mwema juma hili
Post a Comment