Kumekuwa
na hali ya taharuki katika eneo la Tegeta, Namanga karibu na kituo cha
Mafuta cha Big Bon jijini Dar es salaam baada ya wananchi wenye hasira
kuanza kurushiana mawe na Mapanga na watu waliotumwa kubomoa Vibanda
vilivyo katika eneo hilo.Katika tukio hilo watu Wawili wamejeruhiwa vibaya na wamekimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu zaidi.Kwa
mujibu wa Kamanda KENYELA kikundi cha watu kilifika katika eneo hilo na
kuanza kubomoa Vibanda vilivyo katika eneo hilo la Namanga hali
iliyowashtua wananchi wa eneo hilo na kisha kuanza kurushiana Nawe na
Mapanga na kikundi hicho cha watu.Hata
hivyo watu Wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa huo wa
Kinondoni kwa mahojiano zaidi kama wana uhalalali wa kubomoa Vibanda
hivyo na wametumwa na nani.
Loading...
Post a Comment