Social Icons

Loading...

Dr: Fenela apata ajali ya gari akielekea Mwanza

Dr: Fenella   Mukangara
Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni Dokta FENELLA MUKANGARA(pichani) amepata ajali ya gari katika Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora akiwa njiani kwenda Mkoani Mwanza kikazi.Habari kutoka Wilayani Nzega zinasema kwamba ajali hiyo imetokea leo asubuhi wakati Waziri huyo akiwa njiani akitokea Dodoma kwenda Mkoani Mwanza kuzindua Mashindano ya Vishale.Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kwamba gari aliyokuwa amepanda Waziri MUKANGARA akiwa na Msaidizi wake imepinduka mara Tatu na inadaiwa kuwa Waziri huyo ameumia Mguu wa kushoto na amekimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega kwa ajili ya matibabu zaidi.
Chanzo:  Uhuru FM.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

1 comments:

Pole Dr kwa ajali Mungu akuponye

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top