Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema wizara
yake itachukua hatua za haraka ili kudhibiti matumizi ya pombe
zinazowekwa kwenye pakiti maarufu kwa jina la viroba ambazo zinaathiri
afya za Watanzania wengi.Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya
wizara yake bungeni Dodoma jana, Dk Kigoda alisema wizara yake
itawasiliana na wadau mbalimbali ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.Dk Kigoda, ambaye pia ni Mbunge wa Handeni,
aliwataja wadau hao kuwa ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara za Afya na
Ustawi wa Jamii, Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Fedha na wamiliki wa
viwanda vinavyotengeneza pombe hizo. “Tumelipokea suala la matumizi ya
viroba kwa uzito wa hali ya juu na tutatoa uamuzi wa haraka baada ya
kufanya mazungumzo na sekta mbalimbali,” alisema Dk Kigoda.
Alisema wizara yake kwa kushirikiana na wizara
nyingine itatafuta njia mbadala kuepusha madhara kwa wanaotumia viroba
ambavyo alisema vina athari kubwa kiuchumi na kijamii.
Chanzo gazeti la mwananchi.
Chanzo gazeti la mwananchi.
Post a Comment