WANAWAKE wengi hupata tatizo la kukaukiwa maziwa wanaponyonyesha.
Tatizo hili husababishwa na mambo mbalimbali, likiwemo ukosefu wa vyakula vyenye virutubisho muhimu.
Zipo njia mbalimbali zinazoweza kutumika kukabiliana na tatizo hili hasa upande wa vyakula.
Ndiyo maana nimesukumwa kuandaa aina ya chakula, ambacho ni msaada mkubwa kwa wenye tatizo hili.
Leo tutaangalia namna ya kuandaa supu ya samaki aina ya Pweza.
Mlo huu ni tiba nzuri na ya asili kwa mama anayenyonyesha aliye na tatizo la kukaukiwa maziwa.
Mahitaji
Pweza mbichi
Maji lita moja
Chumvi
Ndimu
Namna ya kuandaa
Mwoshe Pweza hadi uhakikishe shombo imekatika kabisa, kisha mkate vipande utakavyo na uweke vipande hivyo katika sufuria safi.
Weka chumvi na ndimu kiasi. Mimina maji ya kutosha, kisha bandika jikoni ichemke kwa muda wa nusu saa.
Hakikisha Pweza amechemka vizuri na supu yake imeiva.
Ikifika hatua hiyo, mlo wako utakuwa tayari, unaweza kuepua na kuandaa.
Supu hii kama nilivyotangulia kueleza awali, inasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza maziwa ya mama.
Kama una tatizo la kukaukiwa maziwa ni vyema ukaanza kutumia aina hii ya supu mara kwa mara.
Endapo atapendelea, mlaji anaweza pia kuongeza viungo vingine kama pilipili hoho, karoti na vinginevyo. Supu hii inaweza pia kunywewa na watu wa rika na jinsia zote.
Makala kwa hisani http://www.mwananchi.co.tz/mwananchi-jumapili/38-johari/25929-mapishisupu-ya-pweza-kwa-mama-anayenyonyesha

Post a Comment