MWALIMU Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma
aliyejifungua watoto watano kwa wakati mmoja kwa njia ya upasuaji mnamo
Mei 25 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo
mjini Songea na watoto hao kuishi kwa muda wa masaa kumi kabla
hawajafariki dunia ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.
Akizungumza na Demashonews kwa njia ya simu Sophia Mgaya akiwa nyumbani
kwake Ruhuwiko mjini Songea alisema alilazimika kuomba kutoka wodini
kwa sababu alikuwa akijisikia uchungu anapowaona wanawake wenzake wodini
humo wakiwakumbatia watoto wao baada ya kujifungua huku wa kwake wote
wakiwa wamefariki dunia baada ya kuzaliwa.
Alisema kuwa muda wote aliokuwa hospitalini hapo baada ya watoto wake
kufariki huku akiwa bado anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa
alikuwa akilia muda wote anapowaona wanawake wenzake waliojifungua
wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao hivyo akaamua kuomba
aruhusiwe kutoka hospitalini hapo.
‘’Niliomba kuruhusiwa kutoka hospitali na kwenda kujiuguza kidonda
nyumbani kwa sababu ya uchungu na majonzi niiiyokuwa nikiyapata wodini
hapo ninapowaona wanawake wenzangu waliojifungua wakiwakumbatia na
kuwanyonyesha watoto wao huku wa kwangu wakiwa wameshazikwa”alisema
Bi.MgayaChanzo : http://www.jukwaahuru.com/?p=16011
Post a Comment