Siku chache baada ya Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta
kumhusisha Dk John Magufuli na kundi la urais la mwaka 2015, Waziri huyo
wa Ujenzi, ameibuka na kupinga kauli hiyo, akisisitiza hafikirii
kuwania nafasi hiyo.Waziri Sitta alinukuliwa na gazeti hili juzi
akieleza kuwa wakati ukifika, yeye na rafiki zake Waziri Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dk Magufuli
na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, watachagua mmoja wao
watakayeona anafaa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Alisema
hayo juzi kwenye Kongamano la Mawasiliano katika Nyanja za Digitali la
wanafunzi wa Idara ya Uhusiano na Masoko, Chuo Kikuu cha St. Augustine
(SAUT), Mwanza.
Kabla ya hapo alikuwa amewataja rafiki zake hao
wakati wa hafla ya kuchangia Kanisa Katoliki, Josephine Bakita, Parokia
ya Igoma, Mwanza, Jumapili iliyopita.
Alisema hatagombea tena ubunge mwaka 2015, baada
ya kuwa katika ulingo wa siasa kwa miaka 35 na badala yake ataangalia
namna nyingine ya kuwatumikia wananchi huku akigusia mchakato wa kuwania
urais ambao alieleza anamwachia Mungu.
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1866444/-/12u9pof/-/index.html
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1866444/-/12u9pof/-/index.html
Post a Comment