Mamlaka ya Mawasilino Tanzania, TCRA, imesema watumiaji wa simu
ambazo hazikusajiliwa, watakatiwa mawasiliano ifikapo Juni Mosi mwaka
huu.
Tamko hilo lilitolewa jijiji Mbeya na Mkurugenzi
wa Sheria na Leseni wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nziga wakati wa semina
kuhusu utekelezaji wa sheria mpya ya mawasiliano ya elektroniki na posta
ya mwaka 2010 kwa wadau mbalimbali.Hiyo ni awamu nyingine katika mipango ya TCRA,
kwani awali ilikuwa na kampeni za kuzima mitambo ya analogia nchi nzima
na kuwataka wananchi kuingia katika mfumo wa dijitali ulioanzia katika
Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 31, mwaka jana.
Mikoa mingine iliyoingia kwenye mfumo wa dijitali
ni Arusha, Tanga, Dodoma, Mbeya na Mwanza. Nziga alisema mamlaka hiyo
inasisitiza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa makubaliano kati yake na
watoa huduma za mawasilino ya simu na kufikia usiku wa Juni Mosi, namba
za simu ambazo hazikusajiliwa zitakoma. Mmiliki wake hataweza kuitumia
kupiga wala kupokea siku.
Chanzo gazeti la mwananchi .
Chanzo gazeti la mwananchi .
Post a Comment