WAKATI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwasilisha rai
ya kupunguza gharama za mwingiliano wa simu , Kampuni ya Tigo imekataa
kufanya hivyo kwa madai kuwa itahatarisha uwekezaji wake kwa punguzo la
asilimia 69.
Msimamo huo wa Tigo, umekuja baada ya TCRA
kukutana na wadau wa mawasiliano jana jijini Dar es salaam, ili
kukusanya maoni kuhusu mapendekezo ya kupunguza gharama ya mtandao mmoja
kwenda mwingine. Hatua hiyo inalenga katika kuwasaidia wananchi kumudu
gharama za mawasiliano ya simu.Naibu Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda wa
TCRA, Victor Nkya, alisema punguzo hilo ni la kutoka asilimia 35 hadi
asilimia 69 na kwamba litaanza kutumika Machi mosi mwaka huu na kukoma
Desemba 31 mwaka 2017 .
Nkya alisema punguzo la gharama ya kupiga
mtandao mmoja kwenda mwingine kwa mwaka 2013 litakuwa asilimia 34.92,
mwaka 2014 asilimia 32.40, mwaka 2015 asilimia 30.18, mwaka 2016
asilimia 28.57 na mwaka 2017 ni asilimia 26.96.
Zaidi Fuatilia hapa : http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1668454/-/xkrt34/-/index.html
Post a Comment