Tido Mhando |
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uhai Production Ltd iliyo chini ya
Azam Media, Tido Mhando alisema kuwa mpango uliopo sasa ni kuhakikisha
matangazo ya televisheni na redio yanawafikia wananchi kwa weledi wa
hali ya juu.
Akizungumzia uteuzi wake, Mhando alisema uteuzi
huo umempa changamoto ya kufanya kazi kwa ufanisi ili kuifanya Azam
Media kuwa kampuni bora katika utoaji wa habari na burudani ukanda wa
Afrika.
“Ninayo furaha kubwa kujiunga na Azam Media, pia
na changamoto kubwa zilizopo mbele yetu kuifanya kuwa kampuni pekee ya
televisheni na redio yenye ubora katika kutoa burudani hapa nchini na
ukanda wote wa Afrika,” alisema Mhando.
Mhando aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Mwananchi Communications Limited (MCL), alisema kwa sasa ujenzi wa
studio za kisasa Afrika Mashariki na Kati unafanyika na utakapokamilika,
itakuwa ya aina yake kwa Afrika Mashariki na Kati.
Akizungumzia uteuzi wa Mhando, Mkurugenzi Mtendaji
Mkuu wa Azam Media Ltd, Rhys Torrington alisema uteuzi huo umefanyika
huku wakitarajia makubwa kutoka kwa nguli huyo wa tasnia ya habari
katika kuipeleka mbali Azam Tv.
Tunayo faraja kubwa kwa Tido kujiunga nasi wakati
tunakaribia kutimiza mwaka wetu wa kwanza tangu kuanza kutoa huduma na
Azam Tv,” alisema Torrington.
Post a Comment