Asilimia 70 ya Watanzania wanatunza fedha zao nyumbani badala ya
mfumo rasmi ukiwamo benki na huduma nyingine za fedha, imebainika.
Hayo yamebainishwa kwenye ripoti ya FinScope
iliyotolewa jana na Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Fedha Tanzania (FSDT),
ikionyesha kuwa benki nchini zimeongezeka na kufikia 50.
Utafiti huo uliohusisha watu 8,000 umeonyesha kuwa
asilimia 70.4 ya Watanzania milioni 24.2 wanaostahili kupata huduma za
fedha, hawazitumii kutokana na sababu mbalimbali.
Sababu hizo ni pamoja na ukosefu wa elimu ya
masuala ya fedha, umbali kufikia matawi ya benki au wakala, gharama
kubwa za uendeshaji wa huduma hizo, mazoea ya mfumo wa kijima wa
utunzaji wa fedha, kukosa imani kuhusu usalama wa fedha zao.
Akizindua ripoti hiyo, Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu alisema jana kuwa pamoja na hali
hiyo, kumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta hiyo ukilinganisha na
hali ilivyokuwa miaka minne iliyopita.
Soma zaidi mwananchi .
Soma zaidi mwananchi .
Post a Comment