Social Icons

Loading...

AHLY : KUITOA YANGA NI BAHATI TU



Kocha wa Al Ahly, Mohamed Youssef amesifu umakini na nidhamu ya hali juu ya mchezo ilioonyeshwa na wachezaji wa Yanga na kusema ushindi wa timu yake ulikuwa wa ‘ngekewa’ na si uwezo wa uwanjani.
Al Ahly iliiondoa Yanga kwa penalti 4-3 baada ya mchezo huo kumalizika kwa mabingwa wa Afrika kushinda 1-0 hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa bao 1-1 kutokana na  Yanga kushinda bao 1-0 katka mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.
Katika pambano hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Max jijini Alexandria, mabingwa wa Tanzania, Yanga walicheza kwa umakini katika kujilinda na kushambulia.
Yanga walishambulia wote na kila walipopoteza mpira haraka walirudi golini kwao kujilinda kabla ya kuruhusu bao dakika 71 lililofungwa na Sayed Moawad.
Pia, Yanga mara tatu walipoteza nafasi kushinda mchezo huo wakati wachezaji wake Said Bahanuzi, Oscar Joshua na Mbuyu Twite walipopoteza mikwaju yao ya penalti.
Kocha Youssef alisema mchezo ulikuwa mgumu sana kwetu. Tulitaka kushinda katika muda wa kawaida, lakini haikuwa rahisi kwa sababu hatukuwa makini katika kutumia nafasi.
“Watu wengi walifikiri tutawafunga kirahisi Yanga. Hiyo siyo kweli... ilikuwa timu imara, lakini cha muhimu tumefuzu,” Youssef aliuambia mtandao wa Cafonline.
“Bao letu tumelipata kama bahati ya Mungu tu, pia tunashukuru kwa kiwango cha juu cha kipa wetu Sheriff Ekramy aliyeokoa penalti tatu.”

Tizama  penalti  iliyowapatia  ushindi   mafarao  wa  Misri   :  National  Al  Ahly
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top