Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Benard Membe amesema aliulizwa maswali mazito na Kamati Ndogo
ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho
Bara, Phillip Mangula kuhusu mbio za urais 2015.Akizungumza jana mjini Dodoma muda mfupi baada ya
kuhojiwa na kamati hiyo, Membe alisema kamati hiyo inauliza maswali
magumu kuhusu wanayoyafanya pamoja yanayofanywa na mashabiki wao.
“Kamati inauliza maswali mazito na magumu yanayohusiana na uvunjaji wa maadili ya uongozi wa chama chetu… Kamati ya maadili imejipanga vizuri sana wala msidanganyike, wanauliza maswali mazito,” alisema Membe.
Membe aliongeza kusema aliulizwa mambo makubwa
matatu, kubwa likiwa ni kuibuka ghafla kwa makundi makubwa ambayo
yanazaliwa kila wakati chama hicho kinapokaribia kwenye uchaguzi wa
Rais.
“Kuna mambo makubwa matatu ambayo kamati ya
maadili imeyauliza. Kubwa kabisa ni uzukaji ghafla wa makundi makubwa
ambayo yanazaliwa kila wakati wanapodhani mtu fulani anafaa kuwa
kiongozi.”
Alisema na kuongeza: “Suala la pili nililoulizwa
ni tunafanyaje kukifanya chama chetu kiwe na kundi moja litakalokwenda
mwakani kwenye uchaguzi?”
zaidi soma hapa
zaidi soma hapa
Post a Comment