Social Icons

Loading...

Zitto avitikisa vyama.

Maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kutaka kusitishwa kwa ruzuku kwa vyama vya siasa nchini kutokana na kutowasilisha taarifa za ukaguzi wa matumizi yake, yamevivuruga baadhi ya vyama vilivyotajwa.Vyama vya siasa vinaonekana kutoa matamshi yanayolenga kujinasua katika hoja hiyo, vikiwemo vilivyomshutumu Zitto, kuilaumu Serikali na hata vingine vimediriki kutaka ruzuku hiyo ifutwe kwa maelezo kwamba ni ubadhilifu wa fedha za umma.
Juzi Zitto alisema tangu 2009 Serikali ilitoa kiasi cha Sh67.7 bilioni kama ruzuku kwa vyama tisa vya siasa, lakini vyama hivyo havijawahi kuwasilisha taarifa za ukaguzi hesabu zake msajili kama sheria inavyoagiza. Kwa sababu hiyo, Zitto aliamuru Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kusimamisha utoaji wa ruzuku hadi hapo vitakapowasilisha ripoti ya ukaguzi na makatibu wake wakuu kuhojiwa.
Kwa mujibu wa Sheria namba 5 ya 1992 ambayo ilifanyiwa marekebisho ya Sheria namba 7 ya 2009, Vyama vya Siasa vinawajibika kuwasilisha hesabu zake kwa CAG na ofisi hiyo inaweza kuamua kuzifanyia ukaguzi yenyewe au kuteua mkaguzi.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh aliwahi kusema kuwa utaratibu ambao umekuwa ukitumiwa na vyama hivyo kwa kuteua kampuni binafsi siyo sahihi na ni kinyume cha sheria.“Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vinatakiwa viwasilishe hesabu kwa CAG, ndipo tuzikague au tuamue kampuni ya kufanya ukaguzi huo, sasa wao walichagua kampuni binafsi moja kwa moja zikawafanyia ukaguzi,” alisema Utouh wakati akitangaza kuthibitisha ubora wa hesabu za vyama vitano vilivyoshiriki kwenye Uchaguzu Mkuu wa 2010.
Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alipendekeza kufutwa kwa ruzuku hiyo kwa vyama vya maelezo kuwa ni inawanyonya wananchi.“Badala ya kuvipa vyama vya siasa ruzuku, tuelekeze fedha hizo kwenye miradi mingine ya maendeleo,” alisema Mtikila huku akiahidi kwamba chama hicho kitawasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa taarifa yake ya fedha iliyokaguliwa katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa.
chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Zitto-avitikisa-vyama/-/1597296/2035700/-/ewbfygz/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top