Rais Barack Obama amechelewesha kutoa uamuzi wa kuivamia Syria kijeshi baada ya kuazimia kulipeleka suala hilo bungeni ili liidhinishwe.Obama amechukua hatua hiyo wakati huu ambapo shinikizo la kuishambulia Syria na kumwondoa madarakani Rais Bashar al-Assad likizidi kushika kasi, kwa kile kinachodaiwa kuwa amekuwa akitumia silaha za sumu dhidi ya raia.
Mchakato huo unaendelea huku Rais wa Urusi,
Vladmir Putin akimuonya Obama na kusema uvamizi wa kijeshi wa Syria ni
suala lisilokubalika.Tayari Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
amezishutumu Urusi na China kwa kushindwa kushirikiana na nchi za
Magharibi kumaliza umwagaji damu nchini Syria na kuzilaumu kwa
kudhoofisha jukumu la Umoja wa Mataifa.
Katika mahojiano na gazeti moja la Ujerumani
yaliyochapishwa juzi, Merkel alizishutumu Urusi na China kwa kutatiza
juhudi za nchi za Magharibi za kuutatua mzozo wa Syria.
Nchi hizo mbili ambazo ni wanachama wa kudumu
katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walitumia kura yao ya
turufu kupinga maazimio mara tatu kuihusu Syria tangu vita vizuke nchini
humo zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Urusi na China zinatarajiwa pia wakati huu kupinga
azimio linaloungwa mkono na Marekani na Uingereza lililowasilishwa
katika baraza hilo ambalo ndilo lenye mamlaka ya kuidhinisha hatua za
kijeshi dhidi ya utawala wa Syria kutokana na madai ya matumizi ya
silaha za kemikali siku kumi zilizopita viungani mwa Mji Mkuu Damascus.
Chanzo mwananchi
Chanzo mwananchi
Post a Comment