Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Nchini (Necta), Dk Joyce
Ndalichako amesema karatasi za majibu ambazo wamekuwa wakizipata kutoka
kwa wanafunzi zinaonyesha kuwa, watoto wengi wanahudhuria shuleni lakini
hakuna wanachojifunza.
Dk Ndalichako aliyasema hayo jana jijini hapa
alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa mabaraza ya mitihani ya Afrika,
ambao umejikita kujadili suala la tathimini ya elimu kwa nchi za Afrika.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Ndalichako kuzungumza
tangu Serikali itangaze kufuta matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 na
kutaka yapangwe upya, suala ambalo lilipingwa na wadau wengi wa elimu.
Alisema kuwa wakati nchi nyingi za bara hili
zikiwa zimejitahidi kuongeza upatikanaji wa elimu kwa watu, ubora wa
elimu unaendelea kuwa tishio kwa watu wa bara hili kwa vizazi vijavyo.“Kama mabaraza ya mitihani, tumekuwa tukiona
karatasi za majibu kutoka kwa wanafunzi ambazo zinaonyesha kwa uwazi
kabisa kuwa watoto wanahudhuria shuleni lakini hakuna wanachojifunza,”
alisema Dk Ndalichako.
Chanzo gazeti la mwananchi
Post a Comment