Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya Tanzania International
Petroleum Reserves Limited (Tiper), imekabidhi hundi ya Sh1 bilioni kwa
Waziri ya Fedha, Dk William Mgimwa, ikiwa ni kama gawio la Serikali
mwaka unaoishia Desemba 31, 2012.Kampuni hiyo inamilikiwa kwa pamoja kati ya
Serikali yenye hisa asilimia 50 na Kampuni ya Uswisi ya Oryx Oil and
Gas (OOG) yenye idadi hiyohiyo ya hisa.
Akikabidhi hundi hiyo kwa Dk Mgimwa jana,
Mkurugenzi Mtendaji wa Tiper, Daniel Belair, alisema gawio hilo litakuwa
chachu ya maendeleo ya uchumi nchini.“Tunayo furaha kukabidhi hundi hii yenye thamani
ya Sh1 bilioni, ikiwa ni wajibu wetu kisheria kama kampuni. Tunaamini
mchango wetu utasaidia kuchochea uchumi wa taifa,” alisema Belair.Alisema Tiper inatarajia kuongeza zaidi uwezo wa
kuhifadhi mafuta na kufikia zaidi ya lita za ujazo 290,000 ifikapo mwaka
2015, baada ya uwekezaji Dola 12 bilioni za Marekani.Belair alisema hivi sasa Tiper ina kituo kikubwa
cha kuhifadhi mafuta nchini, chenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita za
ujazo 141,000 ikilenga kufikia lita za ujazo 215,000.“Katika uwekezaji mpya, tangi mbili zenye uwezo wa
kuhifadhi lita za ujazo 36,600 zimeshaongezwa katika robo ya kwanza ya
2013,” alisema Belair na kuongeza:“Kipaumbele chetu kikubwa ni kuhakikisha kuwa bidhaa za mafuta ya petroli zinapatikana katika soko muda wote.”
Chanzo mwananchi
Chanzo mwananchi
Post a Comment