Social Icons

Loading...

OBAMA ATUA DAR.

Rais Barack  Obama   wa   Marekani aliwasili Dar es Salaam jana mchana ikiwa ni nchi ya mwisho katika ziara yake barani Afrika ikitanguliwa na Senegal na Afrika Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Rais Obama alisema aliainisha mambo hayo wakati alipozungumza na mwenyeji wake huyo.

Alisema katika mazungumzo hayo, waligusia mradi wa mkubwa wa umeme uitwao Power Afrika wenye lengo la kuongeza kiwango cha umeme kinachozalishwa nchini na barani Afrika ili kupata umeme nafuu na wa uhakika utakaochagiza kuongeza uzalishaji na kukuza ajira.Nchi nyingine za Afrika ambazo zitanufaika na mpango huo ni Kenya, Ghana, Liberia, Nigeria na Ethiopia.Rais Obama alisema pia wamezungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo, ukuzaji wa demokrasia na utawala bora. Alimzungumzia pia mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hashimu Thabeet anayecheza katika Ligi Kuu ya Marekani (NBA), akiwa na timu ya Oklahoma Thunder ya Marekani, akisema hawakuzungumzia suala lake na kuahidi kufanya hivyo siku nyingine.Akijibu swali iwapo anaridhishwa na misaada ambayo nchi yake inatoa kwa Tanzania, Rais Obama alisema anafarijika kwa matunda yanayopatikana katika mapambano dhidi ya malaria, barabara mpya zinazojengwa na katika maeneo mbalimbali ya nchi.“Hatutoi dawa, bali tunajenga miundombinu ya afya, hatutoi chakula, bali kuwezesha nchi kujitosheleza kwa chakula pia tunasisitiza kubadilishwa kwa sheria mbalimbali ili kutoa fursa kwa sekta binafsi kuleta mitaji yao kwa wingi zaidi, lakini jambo la muhimu ni kuijenga Afrika,” alisema.



author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top