Social Icons

Loading...

Serikali yajipanga kudhibiti viroba.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema wizara yake itachukua hatua za haraka ili kudhibiti matumizi ya pombe zinazowekwa kwenye pakiti maarufu kwa jina la viroba ambazo zinaathiri afya za Watanzania wengi.Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake bungeni Dodoma jana, Dk Kigoda alisema wizara yake itawasiliana na wadau mbalimbali ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.Dk Kigoda, ambaye pia ni Mbunge wa Handeni, aliwataja wadau hao kuwa ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara za Afya na Ustawi wa Jamii, Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Fedha na wamiliki wa viwanda vinavyotengeneza pombe hizo. “Tumelipokea suala la matumizi ya viroba kwa uzito wa hali ya juu na tutatoa uamuzi wa haraka baada ya kufanya mazungumzo na sekta mbalimbali,” alisema Dk Kigoda.
Alisema wizara yake kwa kushirikiana na wizara nyingine itatafuta njia mbadala kuepusha madhara kwa wanaotumia viroba ambavyo alisema vina athari kubwa kiuchumi na kijamii.
Chanzo   gazeti  la  mwananchi.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top