Social Icons

Loading...

Facebook, mitandao ya kijamii huathiri watu kisaikolojia .

Facebook, mitandao mingine ya kijamii pamoja na huduma ya ‘blackberry mesenger’ maarufu kama BBM huathiri watu kisaikolojia, husababisha ndoa kuvunjika pamoja na usaliti katika uhusiano, wanasayansi wamebaini.Utafiti huo uliofanywa mwaka 2012 na wanasayansi wa nchini Israel umebaini kuwa kwa wastani, wanawake wanatumia dakika 81 katika mitandao ya kijamii kwa siku ukilinganisha na wanaume ambao hutumia dakika 64, huku watu wasio na elimu wakionekana kuathirika zaidi na mitandao hiyo.Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Tel Aviv walihusisha matukio kadhaa ya kisaikolojia kati ya watu walioathirika na mtandao na udanganyifu uliosababishwa na uhusiano unayoanzishwa kupitia mitandao ya kijamii.Utafiti huo ulibaini kuwa wote waliohusishwa walikuwa na tatizo la upweke, ingawa hakuna aliyekuwa na historia ya matumizi ya dawa za kulevya au matatizo ya kisaikolojia.Watu wenye upweke walionekana kupendelea kutafuta uhusiano kupitia mitandao, jambo linaloelezwa kusababisha kuwaumiza watu hao na kuhisi kusalitiwa.
Kiongozi wa utafiti huo Dk Uri Nitzan kutoka Chuo Kikuu cha Sackler mchepuo wa Tiba na Afya ya Akili, Shalvata Mental Health Care Centre alisema: “Kama ilivyo matumizi ya mtandao yanazidi kuwa makubwa. Vivyo hivyo inavyozidi kuhusiana na masuala ya saikolojia. Mawasiliano ya kompyuta kama Facebook na makundi ya mawasiliano yaliyopo ndani ni sehemu muhimu ya habari hii.”
Chanzo   http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Facebook--mitandao-ya-kijamii-huathiri-watu-kisaikolojia-/-/1597592/1849998/-/tl3712z/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top