Uhuru Kenyatta jana aliapishwa kuwa Rais wa Nne wa Jamhuri ya Kenya, huku akiahidi kutilia mkazo kudumisha amani na umoja.
Akihutubia halaiki ya Wakenya walihudhuria hafla hiyo kwenye Uwanja wa Michezo wa Moi, Kasarani wakiwamo wakuu wa nchi na wawakilishi wa Serikali mbalimbali za kigeni, Rais Uhuru alisema ataongoza kwa haki kwa kuwapa nafasi waliomchagua na ambao hawakumpigia kura.Rais Kenyatta aliapishwa jana baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika Machi 4, mwaka huu kwa kura 6,173,433 ikiwa niasilimia 50.51 ya kura 12,338,667 zilizopigwa. Raila Odinga, ambaye alikata rufaa kupinga matokeo hayo na kushindwa, alifuatia kwa kupata kura 5,340,546 sawa na asilimia 43.70.
“Amani na umoja havitadumishwa hivihivi tu,
bali vitakuja kwa wananchi wote kupatiwa fursa sawa za kiuchumi,”
alisema Kenyatta, ambaye pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi
waliotangulia wa taifa hilo akiwamo baba yake, Jomo Kenyatta, Daniel
arap Moi na Mwai Kibaki, ambaye alikabidhi madaraka jana.Kenyatta (51), ameweka rekodi ya kuwa Rais
mdogo zaidi wa Kenya, pia aliwashukuru wapinzani wake kwa kushiriki
kuimarisha demokrasia.
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1744056/-/129wfet/-/index.html
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1744056/-/129wfet/-/index.html
Post a Comment