Social Icons

Loading...

Robert Lewandowski 4 Christiano Ronaldo 1

 Borussia  Dortumond  4     Real   Madrid  1

Mshambuliaji wa Dortmund Robert Lewandowski ndio mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne dhidi ya Real Madrid katika historia ya ligi ya mabingwa wa ulaya.

* Ilikuwa ni mara ya 10 kwa mchezaji mmoja kufunga mabao zaidi ya manne katika mechi moja ya Champions League. Lionel Messi pekee ndio mchezaji aliyefunga mabao manne mara mbili katika mechi 2 za ligi ya mabingwa wa ulaya.

* Huu ndio msimu wa kwanza ambapo timu zimeruhusu nyavu zao kuguswa mara 4 katika mechi za hatua ya kutoana kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya. Bayern 4-0 Barcelona, Dortmund 4-1 Real Madrid.

* Cristiano Ronaldo nae ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 3 kufunga kwenye mechi sita mfululizo za ligi ya mabingwa ulaya, wengine waliofanya hivyo ni Chamakh na Burak Yilmaz.

* Ronaldo amekuwa mchezaji wa tano kuweka rekodi ya kufikisha mabao 50 ya Champions League. Akiwafuatia Raul 71, Lionel Messi 59, Ruud van Nistelrooy 56 and Thierry Henry 50.

* Timu pekee iliyowahi kugeuza matokeo baada ya kufungwa 4-1 katika mchezo wa kutoana wa Champions League ni Deportivo La Coruna ambao walifungwa 4-1 na AC Milan katika mechi ya kwanza jijini Milan lakini wakaenda kushinda 4-0 kwao Hispania.

* Katika historia michuano ya ulaya ya klabu kumekuwepo na fainali moja tu iliyowakutanisha timu kutoka Ujerumani. 1979-80 UEFA Cup, Frankfurt wakiwafunga Borussia Moenchengladbach.
Taarifa kwa  hisani  ya  blog  ya   Shaffih.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top