Mamlaka ya Udhibiti wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra),
imepandisha nauli za daladala, mabasi ya kwenda mikoani, usafiri wa reli
na tozo za majini kuanzia Aprili 12, mwaka huu.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Sumatra, Ahmad Kilima alisema jana kuwa nauli za daladala zimeongezeka
kwa asilimia 24.46 kwa kuzingatia maoni ya wadau na gharama za
uendeshaji.Kwa upande wa usafiri wa daladala nauli
zimepanda kwa umbali tofauti kutoka Sh300 hadi 400, Sh350 hadi 450,
Sh500 hadi 600, Sh650 – 750 na kwa wanafunzi kutoka Sh150 hadi 200
katika sehemu yoyote watakayokwenda.Nauli za usafiri wa mabasi makubwa ya masafa
marefu nauli hizo zimeongezeka kwa viwango tofauti. Mathalan kwa basi la
kawaida kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya ni Sh30,700, njia ya vumbi
kutoka Kigoma hadi Sumbawanga Sh25,400 na basi la hadhi ya kati (Semi
Luxury) kati ya Dar na Mwanza ni Sh61,400, wakati basi la hadhi ya juu
(Luxury) kati ya Dar na Arusha ni Sh 36,000.Kilima alisema: “Kuanzia Aprili 12 mwaka huu,
kati ya kilometa 0 hadi 10, nauli ya daladala itakuwa Sh400 badala ya
Sh300 zinazolipwa hivi sasa.
“Pia nauli za mabasi ya kwenda mikoani zimeongezeka kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida, mabasi ya kati kwa asilimia 16.9 na mabasi ya daraja la juu kwa asilimia 13.2,” alisema.
“Pia nauli za mabasi ya kwenda mikoani zimeongezeka kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida, mabasi ya kati kwa asilimia 16.9 na mabasi ya daraja la juu kwa asilimia 13.2,” alisema.
Post a Comment