Arusha. Lema aliyekamatwa usiku wa manane kuamkia
Ijumaa wiki hii, alihojiwa kwa saa tatu mfululizo katika Kituo Kikuu cha
Polisi, Arusha lakini alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba kuachiwa
kwake kungehatarisha amani.
Akizungumza na gazeti hili kabla ya kujisalimisha
kwa askari hao usiku huo wa kuamkia juzi, Lema alithibitisha kuwapo kwa
polisi nje ya nyumba yake:
“Wapo nje ya nyumba yangu, wanatishia kupiga
mabomu kama nisipotoka nje, lakini wanajadiliana na walinzi wangu na
mimi nimewataka wanipe hati ya kunikamata,”alisema.
Wakili wa Lema, Humphrey Mtui alisema mahojiano ya
mteja wake na polisi yalidumu kwa zaidi ya saa tatu kuanzia saa 7:50
mchana hadi saa 11:15 jioni, na kwamba walitaka ufafanuzi kwenye hoja
tatu walizodai kwamba zilijengwa kwenye kauli alizotoa Lema wakati
alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA).
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1760426/-/12b2syx/-/index.html
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1760426/-/12b2syx/-/index.html
Post a Comment