MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), jana alianza
rasmi kazi ofisini kwake huku akiahidi kushirikiana na viongozi wa
Serikali wa Wilaya na Mkoa wa Arusha, kusukuma mbele gurudumu la
maendeleo na kutatua kero za wananchi.
Hata hivyo, mbunge huyo alionya kuwa ushirikiano
wake na viongozi wa Serikali katika mambo ya msingi yanayohusu maslahi
na faida ya umma, hautaathiri harakati zake za kupigania haki na kupinga
uonevu, dhuluma na unyanyasaji unaofanywa na viongozi wa Serikali na
vyombo vya dola.
“Nitatimiza wajibu wangu kama mbunge pamoja na
madiwani wote wa Chadema kwa kushirikiana na viongozi na watendaji wa
Serikali, kutatua kero na shida za wananchi. Lakini ushirikiano huu
utafanyika bila kupuuza haki za pande zote,” alisema
Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
Post a Comment