CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza mkakati wa
kuhakikisha kinashinda Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ili kukiwezesha
kuingia Ikulu.
Kimesema kitatekeleza hatua hiyo pia kwa kufanya
uchaguzi wa kuwapata viongozi wake wapya akiwamo mwenyekiti wa taifa,
uchaguzi utakaofanyika ndani ya mwaka huu. Hata hivyo, tarehe, mwezi na
ratiba kamili ya uchaguzi huo itatolewa baadaye.Kujipanga kwa chama hicho sambamba na kujenga hoja
kulithibitika pia katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
mwaka jana mkoani Dodoma, baada ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete
kuwataka mawaziri na makada wa chama hicho kufanya mikutano ya hadhara
na kutumia vyombo vya habari kujibu hoja za wapinzani, badala ya
kutegemea nguvu za Jeshi la Polisi.Katika mkutano huo, Rais Kikwete alimtaja wazi
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, akidai kuwa aliwahi
kumzulia uongo pamoja na mwanaye Ridhiwani.Rais Kikwete alisisitiza kuwa hiyo ndiyo kazi ya
upinzani, akiwaita watu wazima ovyo na kudai kwamba wanasema uongo mbele
ya wananchi na kwamba hata wakati mwingine hunukuu takwimu za uzushi
kwenye vyombo vya habari.
Habari zaidi soma : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1676464/-/bo2cgpz/-/index.html
Post a Comment