MBUNGE wa Jimbo la Iringa ,Mchungaji Peter Msigwa amewataka
wakazi wa Kijiji cha Kigonzile, katika Manispaa ya Iringa kutomchagua
katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ikiwa hatatimiza ahadi ya kuwapelekea
maji na barabara katika kipindi hiki cha uongozi wake.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kigonzile juzi, Msigwa
alisema amepania kuwafikishia maji na barabara wakazi wa kijiji hicho
ili kuwapunguzia kero ya kutafuta maji na adha ya usafiri.
“Ninajua kero ya maji na barabara ndizo zinazowatesa wakazi wa kijiji hiki hususani wakina mama, lakini niseme tu kwamba suala la maji, nimefurahi kuna mfuko mnaendelea kuuchangia deni lililobaki ninalimalizia sasa na kuhusu barabara tayari nimeshaleta greda nitahakikisha barabara hii inatengenezwa, nisipotimiza ahadi hizi msinipigie kura mwaka 2015,”alisema Msigwa.
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1662934/-/vk5saf/-/index.html
Post a Comment