NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (pichani)
anadaiwa kumiliki kampuni inayojishughulisha na masuala ya utalii
kitendo ambacho kinamwingiza kwenye mgongano wa kimasilahi.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyalandu
anamiliki Kampuni ya Nitoke Safaris Ltd jambo ambalo limeelezwa kuwa ni
kinyume na Kanuni za Utumishi wa Umma hasa kwa kuwa yeye msimamizi wa
sekta hiyo.Taarifa kutoka kwa Wakala wa Usajili wa Kampuni na
Leseni (Brela), zinaonyesha kuwa wamiliki wa Kampuni hiyo ni
L.S.Nyalandu na Faraja G. Nyalandu, huku kila mmoja akimiliki asilimia
30 ya hisa.Kampuni hiyo ilisajiliwa Aprili 24, 2009 na kupewa
nambari 70735, wakati huo Nyalandu akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini,
wadhifa alioupata kuanzia mwaka 2000.
Ofisi za kampuni hiyo ziko PPF Complex Suit, namba
24 Barabara ya Mzingo, Arusha na magari ya kampuni hiyo yamekuwa
yakibeba watalii mkoani Arusha.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana akiwa Mwanza,
Waziri Nyalandu alikiri kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo lakini
akasema tayari alishajitoa.
Katika kujenga hoja ya utetezi wake, Nyalandu
alisema kama ambavyo haipendezi yeye kumiliki kampuni ya utalii akiwa
waziri wa wizara hiyo, haitapendeza pia waziri wa habari kumiliki
gazeti.
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1644980/-/11ptvso/-/index.html
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1644980/-/11ptvso/-/index.html
Post a Comment