KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict wa 16, kwa
mara ya kwanza ametuma ujumbe usiotarajiwa katika akaunti yake ya
mtandano wa kijamii wa Twitter.
Papa alionekana akibonyeza vitufe vya ipad yake na kuandika ujumbe unaosema: “Marafiki wapendwa, nimefurahi kuwa karibu nanyi katika Twitter. Asanteni kwa ushirikiano wenu. Nawabariki wote kutoka moyoni mwangu.”
Msemaji wake alisema kuwa mwanzoni Papa alimfikia kila mtu kwa kutumia akaumti zake za lugha ya Kiingereza.Akaunti za Papa za Kiingereza zina zaidi ya wafuasi 660,000. Hata hivyo akaunti za Papa @pontifex zinazomaanisha ‘Papa’ au ‘Mjenzi wa daraja’ zinafuatana kila moja.
Mwaka jana, Papa alituma ujumbe wake wa kwanza Twitter kutoka katika akaunti ya Vatican na kufungua utukufu wa kuona taarifa mpya kutoka tovuti nyingi.
Kiongozi huyo wa dunia wa watu bilioni 1.2 na zaidi walio waumini wa madhehebu ya Romani Katoliki, anatarajia kujitoa kuliko kuandika ujumbe wa Twitter kwa kila mmoja.
Chanzo : http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=43475

Post a Comment