ALIYEKUWA Mbunge wa Njombe Magharibi (CCM), Yono Kevela
amemtuhumu Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula kwa kuvuruga uchaguzi
wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya chama hicho, Wilaya ya
Wanging’ombe kwa kuwabeba baadhi ya wagombea.
Katika madai yake ambayo ameyakatia rufani, Kevela amesema katika uchaguzi huo uliofanyika Julai 29 mwaka huu, mbali na kuwabeba wagombea hao, Mangula alishiriki kutengeneza makundi ya vitisho, rushwa na lugha za kejeli dhidi yake.

Alisema siku ya uchaguzi akiwa amekaa meza kuu,
Mangula alipopewa nafasi ya kuhutubia, aliwaambia wajumbe kuhakikisha
Kevela na mgombea mwingine Hamisi Nurdin hawapiti.
“Mangula alisema watu hao wasichaguliwe kwa kuwa
wana malengo tofauti na yale ya kukitumikia chama,” alidai Kevela.
Malengo yaliyodaiwa katika rufani hiyo ni kuwa Kevela anautaka ubunge wa
Njombe Magharibi na Nurdin ana nia ya kutaka Makao Makuu ya Wilaya ya
Wanging’ombe yawe Igwachanya.
Rufani hiyo imetaja tuhuma nyingine dhidi ya
Mangula kuwa ni timu yake kutangaza kuwa Kevela amejitoa kwenye
uchaguzi… “Hili liliathiri pia ushindi wangu katika uchaguzi huo.”
Rufani hiyo ya Kevela nakala yake imepelekwa kwa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa CCM, Idara ya Usalama na Maadili ya CCM, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho na Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe.
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1640446/-/bq154ez/-/index.html

Post a Comment