Na Meshaki Maganga toka IRINGA:
Wiki ya jana imekuwa wiki ya kazi nyingi na
pilika za hapa na pale. Wiki hii nimebahatika kukutana na rafiki zangu ambao
kwa muda mrefu tumekuwa tukiwasiliana kupitia mitandao ya kijamii na blog bila
kuonana, kuna mmoja ambae aliamua kufunga safari kutoka Dar es slaam mpaka Iringa kuja kujifunza uwekazaji kwenye
mashamba ya miti na mboga mboga. Na ameamua kuwekeza kwa kununua ekari kumi za
kupanda miti. Wiki hii nimejifunza kwamba, kila mtu ana uwezo wa kuchagua
kufanya yale ayatakayo maishani, Dunia ina mengi ya kuyafanya na kuna kila nafasi kwa
mwanadamu yeyote anayechagua kuwa anavyotaka maishani. Chagua maisha unayotaka
kuyaishi na uyaishi kweli.
Usiogope kujaribu kitu, maisha ya
kuogopa kufanya kitu ni maisha yasiyo na maana. Usikubali maisha ya ‘ukawaida’ na ambayo yatakufanya
usiishi maisha makubwa unayostahili.
Siri
kubwa ya watu wenye mafanikio duniani, ni kuwa hawaogopi maisha, wapo tayari kuumia
kwa kuchagua maisha wayatakayo. Chagua kipengele mojawapo cha
kijasiriamali unachotaka kukifanya na
ukifanye kweli kwa moyo wote. Jiendeleze kila siku katika ulilochagua kiasi
ambacho utavunja mipaka na kuweka rekodi yako. Chagua kufanikiwa.
Wewe kama binadamu na sisi
wengine wote, tuna mawazo ya aina moja tu hatuna aina zaidi ya moja. Lakini
haya mawazo yetu yana sifa au tabia kuu mbili. Sifa hizi mbili zinatofautiana
kabisa kana kwamba hazihusu kitu hichohicho.
Sifa hizi zimepewa majina
mbalimbali tangu kufanyika kwa ugunduzi wake miaka maelfu iliyopita. Majina
kama mawazo ya kawaida nay a kina, mawazo yaliyo machona yaliyolala, mawazo ya
nje na ndani, mawazo yenye utashi na yasiyo na utashi, mawazo ya kike nay a
kiume, mawazo razini na yasio –razini na majina mengine.Lakini katika makala
hii nitatumia maneno istilahi hizi- ‘mawazo
ya kawaida na mawazo ya kina’ katika
kuzungumzia jambo hili.
Ili tuweze kuelewa vizuri
kuhusu tofauti ya sifa hizi mbili za mawazo yetu ni vizuri nitatoa mfano hapa:- Tuchukulie mawazo yako kama
bustani ni kile unachokifikiria (fikra)
kama mbegu ambazo unazipanda kwenye bustani hiyo. Kwenye mawazo yako ya kina,
ndipo mahali ambapo mbegu hizo zinapopandwa, yaani zitakapoota. Baadae mbegu
(fikra) hazaliwa kwenye miili na mazingira yanayotuzunguka.
Tunapofikiria jambo lolote.
Fikira hizo huwa ziko kwenye mawazo yetu ya kawaida. Baada ya kuamini juu ya
kile tunachokifikiri, ndipo ambapo fikira hizo huhifadhiwa kwenye mawazo yetu
ya kina.
Wakati mwingine napengine
mara nyingi huwa hatuna habari kwamba kile tunachokiamini kimehifadhiwa kwenye
mawazo ya kina. Lakini kuhifadhiwa huku ni tofauti na kuhifadhiwa kwa maana ya
kawaida tunayoijua. Mawazo ya kina yanapohifadhi fikira zetu huwa yanazifanyia
kazi kwa kadiri zilivyokuja. Kama ambavyo tumeona kwenye mifano yetu ya awali
kabisa ya mada hii, ni kile ambacho kinaombwa na mawazo ya kawaida.
Tunaposema kile ambacho
kinaombwa na mawazo ya kawaida, tuna
maana ya imani zetu, kile au yale yote tunayoyaamini. Kanuni ya ufanyaji kazi
wa mawazo yetu ya kina ni imani zetu. Hakuna mtu anayeweza kuvunja kanuni hii
kwani ni ya kimaumbile. Kwa hiyo, tunachokatikwa kukifahamu ni maana ya imani,
kwa nini inafanya kazi na kwa namna gani.
Uzoefu wetu maishani,
matukio, hali zetu za hisia na matendo yetu, vyote ni majibu ya mawazo yetu ya
kina kwa mawazo yetu ya kawaida. Siyo kweli kwamba ni kile kitu au jambo
tunaloliamini ndilo lene kupelekea matokeo Fulani kwenye maisha yetu, bali
imani yetu kuhusu kitu au jambo hilo. Unapoamini katika ushirikina au
hofu, matokeo yake yatakuwa ni kulogwa,
kuugua, hofu na kukata tamaa, lakini chenye kupelekea hali hizo siyo ushirikina au hofu, bali inini
yako kwenye hofu.
Mawazo yetu ya kina
yakilishwa imani nzuri, yaani vitu au mambo mazuri, nayo hujibu vitu au mambo
mazuri na yakilishwa imani mbaya nayo huzaa vitu au mambo mabaya. Mawazo haya
huwa hayajui kuchuja au tunaweza kusema hayana “akili” kwani hayachambui kama
imani iliyofikishwa kwake ni mbaya au nzuri, kwani zote huzifanyia kazi kwa
namna moja, yakitaka kufanikisha kile ambacho kimeaminiwa na mawazo ya kawaida.
Watu ambao wana uwezo wa
utumia vizuri mawazo yao ya kina wamefanikiwa sana maishani. Siyo kufanikiwa kwa
mali bali zaidi kwa kuwa na furaha au vyote viwili. Wamekuwa na furaha maishani
kwa sababu fikira zao siku zote zimekuea ni nzuri na wamemudu kufuta fikira
mbaya kwenye mawazo yao. Kwa kufikiri kwao vizuri, mawazo yao ya kina yameweza
kuzaa uzuri – mafanikio na furaha.
Wataalamu wengi wanakubali
sasa kwamba, mawazo ya kina ndiyo ambayo kwa kiasi kikubwa yanabainisha aina ya
maisha yetu. Hapo kabla wanasayansi wengi walikuwa wagumu sana katika kuukubali
ukweli huu, lakini hivi sasa hata madaktari wa taaluma ya utabibu wanakubaliana
na jambo hili.
Nimesoma utafiti wa Dr.
Joseph Murphy ambaye amefanya utafiti wa kutosha kuhusu nguvu ya mawazo yetu ya
kina anayaelezea mawazo haya kama nguvu kubwa alionayo binadamu katika
kumwezesha kuboresha maisha yake, ingawa kwa bahati mbaya binadamu wengi
hatujui kwamba tuna nguvu hiyo.’Unaweza kuyapa maisha yako nguvu zaidi,
uwezo zaidi, mali zaidi, afya zaidi, furaha zaidi na raha ya ziada, kwa
kujifunza namna ya kuwasiliana na kutumia nguvu iliyojificha kwenye mawazo yako
ya kina’,anasema kwenye
kitabu chake cha ‘The power of Subconscious Mind’.
Nguvu
hiyo utaiipata vipi? nitaeleza kwa
kifupi hapa chini na kwa msomaji atakaependa anaweza kuniandikia kupitia barua
pepe yangu.
Kama ambavyo tumesema ni
kwamba kile ambacho hututokea kwenye maisha yetu ni matokeo ya majibu ya
mawazo yetu ya kina kwa kile amacho
mawazo yetu ya kawaida yamekiamini. Tunapofikiri kwa kuamini kwamba,
tumeshindwa, tuna mkosi, tumelogwa au tumekwama, taarifa hizi huenda kwenye
mawazo yetu ya kina na kama tulivyobainisha, mawazo haya huwa yanaifainyia kazi
imani yetu bila kujali kama ina faida kwetu au hapana. Kwa hiyo, ni wazi
yataanza kufanyia kazi imani hizo na matokeo yake yataanza kuonekana sawia au baadaye
kidogo, kwa nguvu au kidogo kidogo. Lakini ni lazima matokeo yatapatikana tu.
Hebu jaribu kuwatazama na
kuwachunguza wale watu wanaoaini kwamba wana mkosi au wale wanaoamini kwamba,
hawawezi. Mara zote utagundua kwamba, watu hawa hawatokwi na ikosi au
hawafanikiwi abadani. Mikosi au kutofanikiwa huko huwajia kwa njia ambayo
huwashangaza hata wao wenyewe. Hii ni nguvu ya mawazo ya kina.
Tunapoamini kuwa tuna mikosi
au hatuwezi, mawazo yetu ya kina kwa kufuatana na kanuni za kimaumbile
hutengeneza mazingira ya kutupatia
mikosi au kushindwa huko kwani mawazo hayo hutoa majibu kufuatana na kile
kinachoenda kwenye mawazo yetu ya kawaida, yaani kile tunachokiamini.
Hebu jaribu kuwatazama na
kuwachunguza wale watu wote wanaoamini kwamba wanaweza na wanaoamimi kwamba
watafanikiwa. Mara zote utagundua kwamba, hatima ya watu hawa ni kufanikiwa na
kumudu. Kinachowezesha hilo siyo kingine bali mawazo yao ya kina ambayo
yamepokea taarifa hiyo kutoka kwenye mawazo ya kawaida ya watu hao, yaani
kwenye imani zao.
Tukitaka kufanikiwa au
kuanguka kwenye maisha yetu ni uamuzi wetu wenyewe. Tukizijaza fikira zetu kwa
mawazo mazuri, yenye kutia moyo, ya upendo na uwezo, ni kkweli tutamudu na
kufanikiwa. Tukiyajaza kwa kukata tama, hofu, kushindwa na kujibeza, matokeo yake
yatakuwa ni ya kutuumiza, kutuangusha na kutuvuruga kwa kila hali.
Ni Lazima tukubali kwamba,
sisi wenyewe ndiyo waumbaji wa maisha yetu kwa njia tuchaguayo kwa kuamini
kwetu. Tukiamini na kujiambia kwa njia ya kutuporomosha, ni Lazima
tutapotomoka. Tukiamini na kujiambia kwa njiaya kutuinua, ni Lazima tutainuka.
Chanzo: http://www.mjengwablog.com/2012/12/chagua-maisha-unayotaka-kuyaishi-na.html
Post a Comment