TIKETI ZA
FAINALI ZA AFCON 2013 KUPATIKANA KWA MTANDAO
Washabiki
wanaotaka kushuhudia Fainali za 29 za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
zitakazofanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini watapata tiketi kwa njia
ya mtandao.
Kwa
mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tiketi kwa ajili ya washabiki
(public tickets) wanaotaka kuhudhuria fainali hizo zitakazoanza Januari 19 na
kumalizika Februari 10 mwaka huu, zitauzwa kupitia mtandao wa www.afcon2013booking@eqtickets.com. Pia tiketi
zitapatikana kupitia simu namba +27 879803000.
Fainali
hizo zinazoshirikisha timu 16 zitachezwa Johannesburg, Nelson Mandela Bay, Mbombela,
Durban na Rustenburg. Mechi ya fainali itachezwa Februari 10 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Soccer City jijini Johanesburg kuanzia saa 2 usiku kwa saa za Afrika
Kusini.
Mechi
ya ufunguzi wa fainali hizo itachezwa Januari 19 mwaka huu ambapo wenyeji
Afrika Kusini (Bafana Bafana) wataumana na Cape Verde kuanzia saa 12 jioni
kwenye Uwanja wa Soccer City.
Angola
na Morocco zitacheza mechi ya pili kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 3 usiku.
Timu zote hizo ni za kundi A. Mabingwa watetezi Zambia wako kundi C na wataanza
mechi yao ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya Ethiopia saa 11 jioni kwenye Uwanja
wa Mbombela. Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria na Burkina Faso.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment