Msanii maarufu katika tasnia ya Maigizo na Uchekeshaji marehemu Hussein Ramadhani Mtioeti (27) almaarufu SHAROMILIONEA aliyefariki kwa ajali ya gari jijini kijijini maguzo, Muheza,Tanga amezikwa leo mchan kijijini kwao. Maziko ya msanii huyu chipukizi aliyeanza kujijengea jina katika tasnia ya sanaa nchini yalijaa mamia kama sio maelfu ya watu wa kada mbalimbali na wasanii lukuki.
Mama yake SharoMillionaire (mwenye blauzi nyeusi) akilia kwa uchungu kwani Sharomillionaire ndiye alikuwa mtoto pekee wa kiume katika familia ya Mzee Mtoity. |
Bestisto wa marehemu Sharomilionea Mzee Majuto akiwa pamoja na wasanii wengine wakijongea makaburini |
Waombolezaji wakiubeba mwili wa marehemu Sharomillionaire kuupeleka katika nyumba yake ya milele |
Mwili wa msanii chipukizi Sharomilionea ukiwa ndani ya Jeneza |
Waombolezaji wakiuweka mwili wa marehemu Hussein Mteity "Sharomilionea" katika kaburi |
Mwili wa Sharomilionea ukiswaliwa kabla ya kuwekwa mavumbini katika nyumba yake ya milele
Post a Comment