MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeiruhusu Jamhuri kufanya
marekebisho katika hati ya sababu za rufaa ya kupinga hukumu iliyomuweka
huru aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1),
Jerry Muro na wenzake wawili, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya rushwa.
Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo jana baada ya
mrufani (Jamhuri) aliyekuwa akiwakilishwa na jopo la mawakili watatu wa
Serikali kuomba kufanya marekebisho katika rufaa hiyo, wakati rufaa hiyo
ilipotajwa.
Baada ya kuridhia maombi hayo, Jaji Dk Fauz Twaib anayesikiliza rufaa hiyo alimpa mrufani huyo siku moja kuwasilishwa mahakamani hati ya sababu za rufaa iliyofanyiwa marebisho. Hivyo aliamuru rufaa hiyo iliyofanyiwa marekebisho iwasilishwe mahakamani hapo leo. Jaji Dk Twaib alipanga kusikiliza rufaa hiyo Februari 12 mwaka 2013, ambapo mahakama itasikiliza hoja za pande zote, kabla ya mahakama kutoa hukumu yake.
Katika usikilizwaji huo mrufani atatoa hoja zake za kupinga hukumu hiyo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyowaweka huru Muro na wenzake, na upande wa wajibu rufaa kujibu hoja hizo. Muro na wenzake, Edmund Kapama maarufu kama ‘Dokta’ na Deogratius Mugassa, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama na kuomba rushwa ya Sh10 milioni, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Post a Comment