TIMU ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeifunga 1-0
dhidi ya Kongo
Brazzaville, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu
na ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za vijana wa umri huo Afrika
zitakazopigwa nchini Morocco mwakani. Kwa matokeo
hayo, Serengeti sasa inahitaji hata sare yoyote katika mchezo wa marudiano wiki
mbili zijazo mjini Brazzaville ili kukata tiketi ya Morocco
mwakani.
Kwa ujumla
Serengeti walipigana katika mchezo wa leo, kwani wapinzani wao walionekana kuwa
bora na wenye uzoefu zaidi yao.
Bao hilo
lilifungwa kwa shuti la mpira wa adhabu na beki Mudathir Yahya Abbas kutoka
umbali wa mita 22 na mpira kabla ya kutinga nyavuni ulimbabatiza beki mmoja wa
Kongo na kumpoteza njia kipa Ombandza Mpea Joe na kujaa
nyavuni.
Tanzania; Peter Manyika Peter, Miza Kriston Abdallah, Mohamed
Hussein Mohamed, Ismail Adam Gambo, Miraj Adam Suleiman, Mudathir Yahya Abbas,
Mohamed Salum Haroub, Joseph Kimwaga Lubasha/Dickson Isaac Ambundo, Hussein
Twaha Ibrahim, Suleiman Hamisi Bofu/Tumaini Baraka Mosha na Farid Mussa
Shah.
Kongo
Brazzaville; Ombandza
Mpea Joe, Tmouele Ngampio, Mabiala Gharlevy, Okimbi Francis, Ondongo Boungena,
Ibra Vinny/Issambey Lonvreve, Binguila Handy, Obassi Ngatsongo, Mohendiki Brel,
Atoni Mavoungou na Biassadila Arei.
Post a Comment