Social Icons

Loading...

Jukwaa la Katiba ‘lamchefua’ Jaji Warioba.

MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema Katiba Mpya itapatikana April mwaka 2014 kama kalenda ya tume hiyo, inavyoonyesha licha ya Jukwaa la Katiba Tanzania kukosoa hata ratiba ya mikutano ya utoaji wa maoni.Amesema Jukwaa hilo linakosoa hata muda wa kufanya mikutano ambayo ni asubuhi na mchana na kuhoji kama jukwaa linataka kazi hiyo inafanyike usiku.
Jaji Warioba alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake na waandishi wa habari.“ Hawa jamaa sasa wanakosoa kila kitu hata ratiba yetu ya kufanya mikutano asubuhi na jioni, hivi wanataka tuwe tunafanya mikutano usiku,” alihoji Warioba.Alisema katiba hiyo itakuwa imekamilika katika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kwamba  muda utakaobaki utatosha kuzifanyia marekebisho sheria zitakazohitajika baada ya mabadiliko ya Katiba Mpya.
        Jukwaa la Katiba Tanzania, Jumamosi iliyopita lilitaka sheria ya mabadiliko irekebishwe, ili mchakato wa kupata Katiba Mpya uendelee baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“Hawa jamaa wa Jukwaa la Katiba nawashangaa sana, wanataka tufuate wanayoyataka badala ya sisi kufuata sheria ya tume, tuna uzoefu wa kazi hii,” alisema Jaji Warioba.
Chanzo :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1624684/-/br6dxxz/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top