MMOJA wa Wenyeviti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa
Azzan Zungu pamoja na makada wengine wa CCM, juzi usiku walikamatwa na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma kwa
tuhuma za rushwa.
Habari zilizopatikana mjini hapa juzi usiku
zinasema, Zungu alikamatwa saa 4.30 katika moja ya vituo vya mafuta
akidaiwa kujaribu kutoa rushwa ya Sh100,000 kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu
wa uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM.
Kamanda wa Takukuru Mkoa
wa Dodoma, Eunice Mmari, jana alikiri kuwakamata baadhi ya watu
wakijihusisha na vitendo vya rushwa akiwamo Zungu.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake, Mmari alidai kuwa vijana wake
walimtia nguvuni Zungu juzi saa tatu usiku katika Hoteli ya Golden Crown
akiwa na wapambe wake wakiendelea kugawa fedha kwa wajumbe wa Mkutano
Mkuu wa Wazazi.
Alisema taarifa za Zungu kudaiwa kugawa fedha hizo
walizipata juzi mchana na kuanza kufuatilia nyendo zake ambazo
zilionyesha kuwa na dalili zote za rushwa.“Tuliweka mitego yetu kila
mahali ndipo tukabahatika kukutana naye katika eneo la hoteli hiyo
akiwa na magari mawili, moja ikiwa ni teksi ya kawaida na nyingine ikiwa
ni Prado ambayo ndiyo ilisadikiwa kubeba pesa,” alisema Mmari.
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1608730/-/vgko9j/-/index.html
Loading...
Post a Comment