UONGOZI wa Yanga umesema utasimama kwenye mstari wa utamaduni wa enzi
wa klabu hiyo kutokuvaa jezi yenye rangi nyekundu, na kwa sababu hiyo
haiko tayari kutumia jezi za wadhamini wakuu wa Ligi Kuu Bara, Kampuni
ya Huduma za Simu ya Vodacom.
Katika kusisitiza msingi wa uamuzi wao, uongozi umesema uko tayari kwa hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yao na hata ikibidi kushushwa daraja lakini siyo kuvaa jezi za Vodacom zenye nembo ya rangi nyekundu.
Tayari Yanga imecheza mechi mbili za ligi bila kuvaa jezi zenye nembo ya Vodacom, huku wadhamini wao wakiwajibu barua yao kwa kusisitiza hawawezi kuondoa nembo hiyo ambayo walikubaliana nayo wakati wa kuingia mkataba wa pamoja.
Katibu mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako, alisema jana pamoja na vitisho kutoka Shirikisho la Soka Tanzanua (TFF) kutaka kuwashusha daraja na kuwatoza faini, hilo haliwasumbui na badala yake watabaki kwenye msimamo wao wa kuheshimu katiba yao inayotambua rangi za kijani, nyeusi na njano.
"Tumeandika barua kwa wadhamini lakini hawajatuelewa na TFF wametishia kutupa adhabu kututoza faini ikiwa ni pamoja na kutushusha daraja.
"Itoshe kusema kwamba, msimamo wa Yanga uko wazi na unaeleweka kwa kila anayefahamu historia ya timu na katiba yake. Hatuwezi kuruhusu rangi nyekundu," alisema Mwalusako.
Mwenyekiti wa Kamati ya ligi Kuu, Wallace Karia alisema kamati yake itasimama kwenye kanunu za kuiadhibu Yanga iwapo itaendelea kukataa kuvaa jezi za mdhamini.
Kauli ya Karia inafuatia msimamo uliotangazwa hivi karibuni na uongozi wa Yanga kuwa kamwe hawatapokea na kuzitumia katika mechi zao jezi zenye nembo nyekundu zinazotolewa na Vodacom.
Kwa hisani ya : http://www.mwananchi.co.tz/michezo/16-kandanda/26458-yanga-tupo-tayari-kushuka-daraja

Post a Comment