Mabingwa wa Kombe la Kagame YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichezesha kwata Mgambo JKT ya Handeni,
Tanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga sasa iwe na pointi sawa na
mabingwa watetezi SIMBA SC , Nusura mabingwa hao wa Vodacom Tanzania wachapwe na vibonde wa ligi hii Polisi ya Morogoro baada ya kulazimisha sare ya 1-1, bao pekee la Polisi lilipatikana katika dakika ya
35 kupitia kwa Mokili Rambo kabla ya Amri Kiemba kusawazisha dakika ya 57. Kwa Upande wa Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0,
yaliyotiwa kimiani na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Didier
Kavumbangu.
Cannavaro alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Oscar
Joshua dakika ya pili kutoka wingi ya kulia, wakati Kavumbangu alimalizia pasi
ya Hamisi Kiiza dakika ya 39.Yanga dakika 34 kupata bao la tatu,
mfungaji akiwa ni Jerry Tegete aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya
Kavumbangu.Katika mechi nyingine, Simba ilitoka sare ya 1-1 Polisi
kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji wakitangulia kupata bao dakika ya
35 kupitia kwa Mokili Rambo kabla ya Amri Kiemba kusawazisha dakika ya 57.
Post a Comment