Miamba ya Soka nchini Tanzania Simba na Yanga jana zilitoshana nguvu katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania maarufu kama Vodacom Premier league, mchezo huo ulikosa msisimko na kujawa na rafu za hapa na pale kiasi cha mchezaji mmoja wa Yanga kupewa kadi nyekundu kipindi cha pili , goli la simba lilipatikana mapema dakika ya tatu kipindi cha kwanza kupitia kwa Amri Kiemba, Mchezaji Said Bahanunzi ambaye kwa hakika alikuwa katika kiwango bora( man of the match) aliisawazishia Yanga kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili.
Loading...
Post a Comment