UTAFITI unaonyesha
kuwa akina mama huwa wanatabia tofauti wakati wa uja uzito na mara baada ya kujifungua. tabia hizi
hutegemea je, ni mimba ya kwanza, au ya pili au ya tatu
Mimba ya
kwanza- Akina mama huanza kuvaa teniti mara tu baada ya kuhakikishiwa na dokta
au nesi kuwa wana mimba.
Mimba ya pili-
wanachelewa sana kuvaa teniti, huendelea kuvaa nguo zao za kawaida mpaka dakika za mwisho.
Mimba ya tatu-
Hakuna tena haja ya teniti maana nguo zao za kawaida kwa wakati huu huwa sawa
tu na teniti.
Jina la mtoto wa kwanza hutafutwa kwa makini tena siku hizi
wamama huwa wanafikia mpaka
kugoogle kabisa ili kupata jina .
Jina la mtoto wa pili
hutokea tu hata ndugu akataja jina la shangazi moja wapo au mama mkubwa au
mjomba linakubalika.
Jina la mtoto wa tatu
litategemea na kituko kitakachotokea wakati huo, anaweza akaitwa Maximo,Obama,
Diamond,Oprah, Rick Ross,Twite, huwa halisumbui. Hata jina la dokta aliyekuwa wa kwanza
kuingia wodini baada ya mtoto kuzaliwa.
Matayarisho ya
mtoto wa kwanza huwa makubwa, mama huweza hata kununua vitabu kama UZAZI BILA
MAUMIVU, na kufanya mazoezi ya kutembea kupumua na kadhalika. Mimba ya pili
hakuna mazoezi , Mimba ya tatu hata mume anaendelea kufanya kazi zake tu bila wasiwasi
mpaka siku ya mwisho.
Nguo za mtoto wa mimba ya kwanza hutayarishwa kwa makini,
kama mvulana nguo za kivulana tu, tena hata kwa kumechisha rangi za mashuka, na
zinapangwa vizuri miezi kabla ya siku ya kuzaliwa. Mtoto wa pili anarithi zile
nzuri zisizo na madoa za yule wa kwanza, mimba ya tatu, mtoto atavaa chochote
walichoacha ndugu zake.
Mama akianza kazi baada ya uzazi wa mtoto wa kwanza, siku ya
kwanza anamuachia dada mtoto, utakuta anapiga simu kila dakika 5 kutoa
maelekezo nini cha kufanya. Kwa mtoto wa pili anahakikisha anamuachia dada
namba yake. Kwa mtoto wa tatu dada anaambiwa apige simu tu kama mtoto anaumwa.
Mama akipata mtoto wa kwanza muda mwingi utakuta anatumia kumuangalia mwanae na
kushangaa vituko vya mtoto. Akipata mtoto wa pili muda mwingi anaangalia yule
mkubwa asije akamfinya au kumchoma na msumari mtoto mpya. Akipata mtoto wa tatu
anahangaika kila mara kuficha vitu vya mtoto mpya visichukuliwe na wale wakubwa.
Post a Comment