Social Icons

Loading...

Bunge kuanza Kesho Mjini DODOMA.

MKUTANO wa Tisa wa Bunge la Muungano unatarajia kuanza kesho Mjini Dodoma, huku ripoti ya Kamati Ndogo ya Bunge iliyoundwa kuchunguza tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge ikisubiriwa kwa hamu kubwa.Tume hiyo inayoongozwa na Hassan Ngwilizi iliundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa ajili ya kuchunguza tuhuma hizo zilizoibuka katika mkutano wa Bunge uliopita. Tuhuma hizo ndizo zilizomfanya Spika kuivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.
Baada ya kuibuka kwa tuhuma hizo, Agosti mwaka huu, Makinda aliunda tume ya wabunge watano kuchunguza tuhuma hizo.Ripoti hiyo inatarajiwa kuwa mtihani mkubwa kwa Spika Makinda hasa ikizingatiwa kwamba ndiye mwenye mamlaka ya kuwasilisha ripoti hiyo bungeni hasa kutokana na kuibuka kwa maneno ya chinichini kwamba kumekuwa na jitihada za kuwasafisha wabunge hasa wa chama tawala.
Hivi karibuni, Naibu Spika, Job Ndugai alikaririwa akisema kuwa mamlaka ya namna ya kuiwasilisha ripoti hiyo yako mikononi mwa Spika Makinda.“Kwa kawaida na kanuni zetu ni kwamba Spika anaweza kuamua kama ripoti hiyo ijadiliwe au iwasilishwe kwa njia ipi, wala hawezi kuingiliwa,” alisema Ndugai.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/kitaifa/-/1597296/1605838/-/2a5458z/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright 2025 Daniel Blog in Contemporary News | Designed By Code Nirvana