Timu ya soka ya Taifa ya Brazil imeendeleza wimbi la ushindi na kampeni yake ya kurudisha ufalme wake wa soka Duniani baada ya kusasambua vilivyo timu ya taifa ya Iraq kwa mabao 6-0 katika mchezo mkali wa kirafiki uliofanyika huko Malmo, Sweden.
Katika mchezo huo Brazil ilimrudisha kikosini nguli wake Kaka (anayekipiga na Real Madrid) baada ya kukosekana uwanjani kwa takribani miaka minne; kutokana na sababu mbalimbali hususani majeruhi.
Kaka ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo kwa timu ya Brazil chini ya kocha Mano Menezes aliwaunganisha vizuri makinda wapya wa Brazil na kufanikiwa kutikisa mabao yao kama ifuatavyo; Oscar alifunga mawili (dakika za 21 na 26), Kaka (47), Hulk (55), Neymar (75) na Lucas (79).
Kaka (jezi namba 8) akipongezwa na Oscar (10 mgongoni) baada ya kuipatia Brazil bao |
Kaka (kushoto) akifurahia ushindi na Rais wa zamani wa Brazil Lula Nancio de la Silva wakishika fulana ambayo Mlokole Kaka alimpa zawadi Rais huyo. |
Brazil 6 Iraq 0
Post a Comment