Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 125 ya kuenea kwa injili tangu Agost 1887 mpaka 2012 katika maeneo ya mashariki na Pwani kazi ambayo iliasisiwa na Mmisionari Jakob Johan Greiner yamefana sana.
Katika maadhimisho haya ambayo yalifikia kilele chake jumapili iliyopita katika Shule ya seminari ndogo ya Kisarawe ambapo Mkuu wa KKKT na Askofu wa KKKT: Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mhe. Baba Askofu Dr. Alex Malasusa aliwaongoza zaidi ya waumini 2500 katika ibada kubwa ambayo pia wachungaji 14 walibarikiwa na kuingizwa kazini.
Maadhimisho haya yamezindua na kuasisi mwanzo mpya wa injili na matendo ya kimitume kwa kuzindua miradi 13 katika maeneo mbalimbali ya mashariki na Pwani ikiwemo Zanzibar. Miradi hii yahusisha mashule, zahanati, mradi wa kituo cha kusaidia watoto wenye ulemavu wa akili, kuzindua makanisa, uzinduzi wa mnara wa jubilee n.k.
Mhe. Baba Askofu Dr. Alex Gehazi Malasusa askofu mkuu KKKT |
"SIJIDHANII KWAMBA NIMEFIKA BALI NAKAZA MWENDO"
Post a Comment