Dar Es Salaam Teknohama Business Incubator(DTBI) kitengo kilichoko chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) kwa kushirikiana na Kampuni za Startup World na Google zimeendesha shindano la wajasiliamali wa kati na wadogo katika sekta ya Teknohama Tanzania yanayofahamika kama Start -up World Pitching Competition 2012 , katika mashindano hayo wajasiliamali wapatao kumi walishindanishwa na mshindi atakayeiwakilisha Tanzania mwakani katika mashindano kama hayo duniani ni Ndg: ANOLD MINDE mjasiliamali aliyetengeneza mfumo wa komputa wa kuratibu tiketi za usafiri wa mabasi ( Bus Reservation Information Systems) hasa yaendayo mikoani ujulikanao kama SAFARI YETU
Mkurugenzi wa COSTECH Dr Hassan Mshinda akifungua mashindano hayoMkurugenzi msaidizi wa DTBi Mr Mramba Manyelo akifafanua jambo wakati wa mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh:January Makamba akitoa hotuba katika shindano hilo na kisha kumtangaza mshindi.
Mshindi Ndg Anold Minde akiwashukuru majaji na waandaji wa shindano hilo.
Jopo la Majaji wakiratibu shindano hilo.
Sehemu ya Washiriki na Wageni waalikwa wakisilikiza na kufuatilia shindano, Ze Blogger naye akisikiliza na kuchukua nondo taratibuuu.
Ndg: Gido Msita toka kampuni ya Blackmark Corporation akiwasilisha mfumo wa komputa ujulikanao kama School Management Information Systems (SMIS) .
Mshiriki toka Victor TechnoSolve Empresa akiwasilisha mfumo wa Control system Incubator
Duuu huyu mdau Bwana Mdogo FOUNDER wa kampuni ya Magila Tech Ltd Ndg : Godfrey Magila akiwasilisha mfumo wa komputa unaomwezesha mtumiaji wa simu ya kiganjani kusikiliza vikao vya Bunge la Tanzania Live ,maarufu kama MOBILE PARLIAMENT SESSION LIVE STREAM SYSTEMS.
Mdau Mary Mgulusi wa mtandao wa HARUSI YANGU website akiwasilisha mfumo wa kuratibu Harusi.
Pascal Maduhu mshiriki akiwasilisha mradi wake wa Mwananchi for Swahili Facebook and Twitter.
Mwakilishi kampuni wa Startup world akimpongeza Ndg: Anold Minde kwa kuibuka mshindi
Post a Comment